Nyota Mpya

NYOTA MPYA

Inua kichwa chako na uwe na moyo mkuu, kwa maana tazama, wakati umekaribia, na usiku huu ishara itatolewa, na kesho naja ulimwenguni.

Na ikawa kwamba maneno ambayo yalimjia Nefi yalitimizwa, kwani tazama, jua lilipozama, hapakuwa na giza; na watu wakaanza kustaajabu, kwa sababu hapakuwa na giza usiku ulipofika.

Na ikawa pia kwamba nyota mpya ilitokea, kulingana na neno. [Na] sehemu kubwa ya watu waliamini, na wakaongoka kwa Bwana. Na Nefi akaenda miongoni mwa watu, akibatiza kwa toba.

Kitabu cha Mormoni, 3 Nefi Sura ya 1, sehemu za aya ya 12 hadi 27

Imechapishwa